WALINZI WA G4S KATIKA MGODI WA GGM GEITA WAGOMA.
Habari na Joel Maduka.
Wafanyakazi
wa kampuni ya ulinzi g4s mkoani geita
wanaofanya kazi katika mgodi wa dhahabu wa GGM, wamelazimika kugoma leo kwa kile wanachodai ni kutokana na kuwepo kwa maslahi madogo
na malipo duni katika kampuni
hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya wafanya kazi wenzake, pascal temba,amesema kuwa kuna mambo manne ambayo yamewalazimu kugoma ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa
uongozi mbaya, mazingira kuwa magumu wanayofanyia
kazi na kupatiwa malipo duni ambayo hayaendani
na mikataba waliyopatiwa.
Aidha
kwa upande wakeEvaryn Raiza,ambaye ni moja kati
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,ameongeza kuwa mgomo huo utadumu endapo kama hautapatiwa ufumbuzi na kutatuliwa matatizo
waliyonayo na yanayoendelea kuwasumbua kwa kipindi kirefu.
Mkuu
wa wilaya ya Geita,Manzie Omary Mangochie,amemaliza
mgomo huo kwa kuwataka wafanyakazi warejee
kazini na serikali kupitia viongozi wa kampuni hiyo watahakikisha
wanazungumza na kufikia makubaliano kwa yale ambayo wamekuwa wakiyadai kutimiziwa katika kazi wanazozifanya.
Wafanyakazi
wa g4s wamerejea kazini na kwamba kutaundwa
kamati ambayo inatarajia kukutana kesho kwa ajili ya
kuzungumza na mkuu wa wilaya kujua hatma na utatuzi wa madai ya wafanyakazi
hao.
Post a Comment