Wakazi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameitaka Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhamishia zoezi la bomoabomoa Wilayani hapa kutokana na baadhi ya wananchi kuvamia na kujenga katika maeneo ya wazi pamoja na yale ya huduma za jamii.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wanaoishi mjini hapa wameitaka serikali kupitia halmashauri ya mji wa Kahama kuendesha zoezi la bomoabomoa kwa wale wote waliovamia na kujenga kwenye maeneo hayo.
Kajolo Mohami anayeishi mtaa wa Nyasubi alisema karibu maeneo yote ya wazi na yale ya huduma za jamii mjini hapa yalishavamiwa na kujengwa na watu wenye fedha hali iliyosababisha kuharibu taswira ya mpango miji.
Alisema anapenda serikali kupitia halmashauri ya mji wa Kahama kuendesha zoezi hilo kama inavyofanyika Jijijini Dar-es-Salaam kwa wale wote waliokuwa wamevamia na kujenga kinyume cha sheria katika maeneo ya wazi.
Nae Peter Samson mkazi wa Majengo mjini alisema agependa kuona bomoabomoa kama inayofanywa na jijini Dar na serikali inafanyika mjini Kahama kutokana na kuwa maeneo yote ya wazi ya huduma za jamii , shule za msingi watu walishayavamia na kujenga.
“Tunapenda kuona zoezi hilo linahamia katika mjui wa Kahama kwani kuna baadhi ya maeneo mengi yamevamiwa na wafanyabiasha wenye fedha na kuwekeza katika ujenzi wa mashule pamoja na ujenzi wa majumba katika maeneo zinapopita barabara hali amabyo imekuwa ni kero kwa Wananchi”. Alisema Samson.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba, aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa mji wa Kahama hauwezi kuendelea na kupata hadhi ya Manispaa bila ya kufanya zoezi la bomobomoa katika baadhi ya maeneo na mitaa yaliyojengwa kinyume cha sheria.
Post a Comment