Header Ads

SEMINA NA MAKONGAMANO KUFANYIKA KWA MTANDAO HAKUNA POSHO TENA.


SERIKALI kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA).

Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.

“Tulianzisha mfumo huo ili kupunguza gharama zisizo na ulazima ambapo awali ilitakiwa kila kunapokuwa na kikao lazma watumishi wasafili kuja Dar es Salaam kwaajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia Video Conference iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. Tumeokoa gharama za nauli, mafuta, chakula na malazi,” amesema Temba.

Temba ameeleza kuwa, hatua za utekelezaji wa teknolojia hiyo ulianza kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2013 hadi sasa ambapo umekamilika na kufanyiwa majaribio yaliyofauli kwa kufanya mikutano kumi ambayo iliunganisha mikoa yote kasoro mitatu ambayo ni mipya ambayo ni, Njombe, Geita na Simiyu.

Kuhusu miondombinu ya mawasiliano amewatoa hofu watumishi kwa kusema: “Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.”

No comments