RAIS KIKWETE AZUNGUMZIA MICHEZO TANZANIA.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliacha kwenda uwanjani kuiangalia timu ya taifa Stars kwa kuwa alionekana kuitia mkosi wa kufungwa timu hiyo kila ilipocheza
Akiongea wakati wa kulihairisha bunge na kuwaaga wabunge, Raisi Kikwete alisema zamani alihudhuria sana mechi za Stars na baada ya kuwa inafungwa, aliamua kutokwenda uwanjani .
“Mwanzoni nilikuwa navaa hadi jezi kuishangilia timu yetu ilipokuwa inafanya vizuri, tulipoanza kufungwa fungwa wakasema mzee unaitia timu mkosi, nikaamua kuacha”, alisema Raisi Kikwete huku akicheka katika hali ya mzaha
“Lakini hata baada ya kutokwenda uwanjani, timu imeendelea kufungwa tu, tusikate tamaa”, alisema Raisi Kikwete mpenda michezo. Taifa Stars imetolewa michuano ya kufuzu ya CHAN na Uganda na sasa ina kibarua cha kufuzu fainali za AFCON mwaka 2017.
Hata hivyo, Raisi Kikwete amewataka Watanzania kutokata tamaa na kufanya vibaya kwa sekta ya michezo na badala yake jitihada za kuendeleza sekta hiyo ziendelee na ipo siku sekta hiyo itafanya vizuri kimataifa.
Amesema serikali yake imefufua michezo ya mashuleni ili kukuza vipaji kwa ajili ya taifa hapo baadae
Amesema serikali yake imeingia ubia na makampuni ya kimataifa yay a Symbion Power na klabu ya Sunderland ya Uingerteza kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambacho kinategemewa kuanza kazi mwezi Septemba.
“Tujitahidi, tusikate tama, tutafika tunapopakusudia”, alisema Raisi Kikwete katika hotuba hiyo ambayo aliitumia kulianga bunge akijiandaa kuachia madaraka mwezi Oktoba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Raisi na wabunge.
Raisi Kikwete amesema serikali yake pia imechukua jitihada za makusudi kuendeleza sekta ta muziki na filamu kwa kuwaalika wataalamu kutoka Marekani kutoa mafunzo ya sekta hizo kwa wasanii wa Tanzania ili wafanye kazi nzuri itakayotambulika kimataifa.
Post a Comment