MOHAMMED DEWJI AWAAGA RASMI WAPIGA KURA WAKE.
Mbunge wa Singida mjini (CCM) na mfanya biashara maarufu nchini Mohammed Dewji ametangaza rasmi kutogombea tena nafasi hiyo kwa madai ya kubanwa na majukumu ya kifamilia na biashara.
Dewji amekuwa mwakilishi wa jimbo hilo kwa vipindi vitatu mfululizo, alisema aliomba ridhaa ya wananchi kuwawakilisha bungeni mwaka 2000 wakati huo biashara yake ilikuwa haijakua na pia hakuwa na familia.
Akiongelea baadhi ya mambo aliyofanikiwa kuyafanya wakati wa uongozi wake Dewji aliyataja kuwa ni pamoja na kujenga shule 15 za sekondari kutoka mbili zilizokuwepo.Pia kwa kutumia fedha zake alichimba visima 45 vya maji safi na salama.
Katika tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na mamia ya watu,wapo pia walioshindwa kujizuia kuonyesha hisia zao kwa kutokwa na machozi kutokana na upendo kwa mbunge wao huyo huku wengine wakimtaka aendelee.
Post a Comment