MKUU WA WILAYA NGARA AJITOSA KUWANIA UBUNGE GEITA.
mkuu wa wilaya ya Ngara Constatine Kanyasu.
MKUU wa Wilaya ya Ngara Bw,Constatine Kanyasu amesema endapo atapewa ridhaa na chama cha mapinduzi (CCM), kugombea kiti cha ubunge jimbo la Geita atahakikisha anatatua changamoto mblimbali ikiwemo maji na maeneo ya wachimbaji wadogo.
Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo jana, wakati wa kurudisha fomu yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Bw, Kanyasu ameongeza kuwa yeye ni mzawa wa Geita hivyo anajua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo la Geita, ambapo amedhamiria kushirikiana nao kikamilifu endapo chama chake kitampitisha na wananchi kumpa ridhaa ya kuwaongoza.
Aidha baadhi ya wazee wakongwe wa CCM waliomsindikiza DC Kanyasu walisema kuwa kabla Kanyasu hajawa mkuu wa Wilaya ya Ngara amefanya mambo mengi kwa kutumia fedha zake bila kujali itikadi za chama.
Post a Comment