Header Ads

MAANDALIZI YA IDD GEITA, POLISI KUIMARISHA ULINZI.


Image result for JOSEPH KONYO
kamanda konyo
JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LIMEWATAKA WANANCHI KUSHEREKEA SIKU KUU YA IDDY   KWA AMANI NA UTULIVU  WAKATI WOTE WA SHEREHE HIZO,AMBAPO KITAIFA ZITAKUWA MKOANI GEITA,HUKU MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMMED GHARIB BILALI AKITARAJIWA KUHUDHURIA SHEREHE HIZO NA VIONGOZI WENGINE WA DINI NA SERIKALI.
AKIZUNGUMZA NA PAUL BAHEBE BLOG,KAMANDA WA MKOA JOSEPH KONYO ,JUU YA UTULIVU WA WANANCHI KATIKA KIPINDI CHA SHEREHE ZA IDDY.
KAMANDA KONYO,AMESEMA KUWA NI VYEMA KWA WANANCHI KATIKA KIPINDI HIKI KUWA WAANGALIFU NA KUSHEREHEKEA KWA AMANI NA KUACHANA NA MAMBO AMBAYO YATAKUWA YANAONYESHA VIASHAILIA VYA UVUNJIFU WA AMANI.

 AIDHA KAMANDA KONYO,AMEWATAKA WAZAZI KUWA WAANGALIZI WAZURI KWA WATOTO NA KUWA NA UKARIBU HUSUSANI MAENEO YA BARABARANI.
JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LIMEJIPANGA VYA KUTOSHA MKOANI HAPA KWA RAIA YEYOTE  ATAONEKANA KUVUNJA AMANI ,ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.PAUL BAHEBE


No comments