Header Ads

CHADEMA GEITA HAKUKALIKI BAADA YA MTIA NIA KUKATWA.

WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)WILAYANI GEITA  WAMETISHIA KUKIHAMA CHAMA  HICHO ENDAPO MTIA NIA WA KITI CHA UBUNGE KUPITIA CHAMA HICHO BW RODGERS LUHEGA HATA PITISHWA  KWENYE  KURA ZA MAONI.
WAFUASI HAO WAKIZUNGUMZA NA  STORM FM WAMESEMA KUWA  KIONGOZI AMBAE WANAAMINI ATAONGOZA VIZURI  NA KULETA MABADILIKO KATIKA MJI WA GEITA NI  RODGERS NA KAMA  LAITI CHAMA HICHO HAKITAMPITISHA MGOMBEA HUYO KUGOMBEA UBUNGE , WAKO RADHI KUKIHAMA  CHAMA CHA CHADEMA.

AIDHA KWA UPANDE WAKE MTIANIA,BW RODGERS LUHEGA,AMEWATAKA WAFUASI HAO KUWA WAVUMILIVU KWANI KULA ZA MAONI KIKAWAIDIA ZINAWATOA WATU WATATU NA KUWAPELEKA KAMATI KUU AMBAPO HUJADILIWA NA KUTOA MGOMBEA MMOJA.

AKITOA MATOKEO YA UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI , MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HUO ,BW COSMAS SHIRATU AMESEMA KUWA JUMLA YA KURA ZILIKUWA 180 NA  WAGOMBEA WALIKUWA SITA WALIOPITISHWA KUPELEKWA KAMATI KUU NI WATATU.
CHANZO/KURA ZA MAONI CHADEMA/JOEL MADUKA/24JULAI2015



           Rodgers Luhega anayewania ubunge kupitia Chadema anayedaiwa kufanyiwa hila.
                                                  Wafuasi wa Chadema wakipinga matokeo.

No comments