Header Ads

UGANDA: Mkuu wa jeshi aliyempigania Rais Museveni kuingia madarakani atumbuliwa

Tokeo la picha la Kale Kayihura and museveni
Rais Yoweri Museveni na Kale Kayihura
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amemfuta kazi Mkuu wa Jeshi la polisi nchini humo, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.
Generali Kayihura, ambaye alipambana vya kutosha kwenye vita ya msituni dhidi ya Idd Amin na kusaidia Rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, ametumbuliwa kutokana na kudorora kwa usalama wa taifa nchini Uganda.
Kupitia ukurasa wa Twitter Rais Museveni amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika”Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.
Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Uganda, zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha mjini Kampala na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.

No comments