Mbunge wa CCM Mary Nagu akamatwa na polisi kwa amri ya DC
Mhe. Mary Nagu
Mbunge wa Hanang kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Mary Nagu Jumatano hii (March 7) aliangukia mikononi mwa Polisi baada ya kukamatwa akiwa jimboni kwake katika kijiji cha Lalaj Kata ya Lalaj wilayani Hanang.
Mh. Nagu alikamatwa majira ya saa 11:00 jioni kufuatia agizo la mkuu wa Wilaya ya Hanang Sara Ally Msafiri kwa madai kuwa Mbunge huyo alitofautiana maagizo na mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo Mh. Nagu aliachiwa jana hiyo hiyo baada ya uongozi wa CCM Wilaya ya Hanang kuingilia kati kutafuta suluhisho la mvutano huo ambao haujaelezwa ulikuwa unahusu nini haswa.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa ameagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.
Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali
Post a Comment