Header Ads

"WAANDISHI TUMIENI FURSA ZITOLEWAZO NA MASHIRIKA" PROSPER KWIGIZE

Mkufunzi wa Mafunzo kutoka UNESCO Bi. ROSE HAJI MWALIMU

Waandishi wa Habari kutoka Redio za Kijamii Tanzania wametakiwa kutumia fursa
zinazotolewa na Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
–UNESCO- ili kuleta mabadiliko kwa Jamii.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania –TADIO -,
PROSPER KWIGIZE katika mafunzo yanayoendelea mjini DODOMA, yanayoshirikisha
waandishi wa habari 49 kutoka redio 24 za jamii.
Bwana KWIGIZE amesema mafunzo kwa waandishi wa habari hususani katika maeneo
ya mazingira na jinsia hutolewa kwa kulipia kiasi cha ada lakini UNESCO hutoa
mafunzo kama hayo bila malipo yoyote.
Amesema ni vyema kuthamini na kuzingatia elimu wanayoipata waandishi katika
mtandao wa TADIO na kuifanyia kazi kwa manufaa ya jamii.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo ROSE HAJI MWALIMU ametoa wito kwa
waandishi wa habari kutoka redio za kijamii kuibua changamoto zinazochangia kuleta

usawa katika masuala ya kijinsia.

No comments