Tetesi za soka Ulaya Jumapil 11.02.2018
Klabu ya Manchester City imekubali mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk's 24 na raia wa Brazil Fred kwa dau la £44.5m mwisho wa msimu huu. (Goal)
Klabu za Manchester City na Manchester United zina hamu kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire, 24. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 28, analengwa na AC Milan, ambayo iko tayari kutoa dau la £32m kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania.(Tuttosport via Express)
Chelsea huenda ikamuajiri mkufunzi wa zamani wa Hull na Watford Marco Silva kusimamia klabu hiyo kwa muda mfupi iwapo watamfuta kazi Antonio Conte kabla ya mwisho wa msimu huu.. (Times - subscription required)
Mshambuliaji wa Ubelgiji 27, Eden Hazard amesema kuwa katika soka lolote linawezekana kabla ya kuongeze kwamba anafurahia kuichezea Chelsea wakati alipoulizwa kuhusu kuhusishwa kwake na Real Madrid. (Marca)
Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, hajapinga uhamisho kurudi katika klabu yake ya zamani Real Madrid. Alipoulizwa iwapo anaweza kurudi Real Madrid alisema kuwa anafurahia kusalia na Blues lakini akaongezea kuwa ''Madrid ni Madrid''.(Mail)
Real Madrid wanaamini itakuwa rahisi kumsajili kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, mwisho wa msimu huu ikilinganishwa na kipa wa Manchester United David de Gea, 27. (Independent)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ametaja kuwa habari za uongo kuhusu ripoti kwamba klabu hiyo inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania ,25 Isco. (El Pais - in Spanish)
Arsenal na Chelsea wote wanataka kumuajiri kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa meneja wake.. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 26, huenda akabaini kwamba kazi yake katika klabu hiyo imekwisha kufuatia kuwasili kwa aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Dortmund-Emerick Aubameyang, 28, kulingana na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Emmanuel Petit. (sun)
Mkufunzi wa zamani wa Uingereza Roy Hodgson, ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa Crystal Palace, amesema kuwa Wayne Rooney anaweza kufanya kazi nzuri kama mkufunzi kwa kuwa ni mchezaji mwenye haiba ya juu. (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kuwa mkufunzi wa Everton Sam Allardyce alichelewa kuomba msamaha kwa kumkejeli anavyozungumza.. (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Stoke City Paul Lambert anataka klabu hiyo kumpatia mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 26 Xherdan Shaqiri, mkataba mpya .Shaqiri amesalia na miezi 16 katika kandarasi yake (Express)
Wamiliki wa klabu ya Swansea wanasema kuwa rekodi yao katika soko la uhamisho imechanganyika na dirisha la uhamisho la msimu huu lilikuwa baya zaidi. (Guardian)
Beki wa Tottenham Jan Vertonghen, 30, alikataa uhamisho wa kwenda Arsenal wakati alipoondoka Ajax 2012 na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaamini alifanya uamuzi wa busara kujiunga na Spurs.. (Mirror)
Mshambuliaji wa Manchester United striker Marcus Rashford, 20 ana mali yenye thamani ya £2m kufikia mnamo Aprili 2017 ikilinganishwa na £100 mwaka mmoja uliopita. (Sun)Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney anasema kuwa angependelea siku moja kuwa mkufunzi katika ligi ya Uingereza.. (Telegraph)
Post a Comment