Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kulijengea heshima Taifa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Programu ya Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika
Na
Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Serikali
yatao Milioni Mia saba kwa ajili ya ukarabati wa Jengo lilokuwa Makao Makuu ya
Wanakamati wanaopigania Uhuru wa kulikomboa Bara la Afrika ikiwa ni sehemu ya
kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo
ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam kupata taarifa
ya maendeleo ya programu hiyo.
‘’Tumepewa
dhamana na heshima kubwa na Umoja wa Afrika ya kuhifadhi historia ya Ukombozi
wa Bara la Afrika sababu ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alivyopigania
uhuru wa bara la afrika na kutoa ofisi jijini Dar es Salaam ambayo ilikuwa
Makao Makuu ya wapigania Uhuru kutoka nchi mbalimbali za Afrika kukutania na
kupanga mikakati hivyo ni vyema tuhifadhi historia hii,’’ Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika ziara yake ofisini hapo Waziri Mwakyembe alisema serikali
inampango wa kujenga ofisi kubwa na za kisasa katika maeneo ya Bunju Mwabepande
jijini Dar es Salaam ambazo itahifadhi historia yote na hapo patakuwa ni kituo
cha Kimataifa ambacho watalii na wageni mbalimbali watatembelea na kupewa
historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
Kwa
upande wa Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi
Ingiedi Mduma alieleza kuwa kituo hicho kitakachojengwa kitakuwa ni moja
kivutio cha utalii na kitasaidia kuiingizia serikali mapato kutoka na wageni watakao kuwa wakitembelea
kituo hicho na eneo lake linakaribia ekari hamsini.
Pamoja
na haya Mheshimiwa Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania kuhifadhi na kutunza
maeneo yaliyotumika na mashujaa hao waliyokuwa wakipigana kukomboa bara la
Afrika pamoja na kutoa taarifa za maeneo wanayojua yalitumika na mashujaa hawa
kwa lengo ya kuisaidia serikali ili iweze kuhifadhi historia hiyo adhimu yenye
kulipa Taifa heshima kubwa.
Hata
hivyo serikali imeanda muswada utakao pelekwa bungeni kwa ajili ya kupatikana
kwa sheria itakayosimamia vyema historia mbalimbali za taifa letu.
Mratibu
wa Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiahedi Mduma (katikati)
akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (kulia) jengo ambalo lilikuwa ni
Makao makuu ya Viongozi wa Kamati ya kupigania uhuru wa bara la
afrika hapo zamani ambalo linahitaji
ukarabati kwa sasa alipotembelea ofisi
zinazoratibu programu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Post a Comment