Header Ads

Bundesliga kubadili mfumo kukwepa utawala wa FC Bayern

images-3

Nyota wa zamani wa Bayern Munich Stefan Effenberg amesema kuna haja ya kufanya marekebisho ya namna ya uendeshaji wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Kwa kuangalia namna ligi ya Bundesliga imekuwa kwa siku za hivi karibuni Bayern imeendelea kutawala na itaendelea kutawala kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha ukilinganisha na vilabu vingine unaompa uwezo wa kusajili wachezaji wengi wazuri.
Effenberg yeye amependekeza uundwe mfumo mpya utakaofanya Bundesliga kuwa na mvuto na ushindani kama miaka ya nyuma.
Kwa misimu mitano nyuma ligi hiyo ilikuwa na mvuto hasa kipindi cha Dortmund ya Jurgen Klopp kidogo walijaribu kuleta ushindi lakini kwa sasa Bayern inayongoza ligi kwa tofauti ya pointi 18 na Bayer Leverkusen iliyopo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Misimu ya hivi karibuni Bayern imekuwa ikitangaza ubingwa mwezi wa pili au wa tatu wakichelewa sana basi ni mwezi wa nne, sasa imeonekana hii salama sana kwa afya ya soka la Ujerumani kwa sababu Bayern pekeake wakiendelea kutawala soka la Ujerumani litaporomoka.
Effenberg amekuja na hoja kwamba, timu 18 zigawanywe katika makundi mawili ya timu tisa kwa kila kundi wacheze nyumbani na ugenini halafu timu nne za juu kila kundi zinafuzu kuingia raundi ya pili pamoja na timu moja yenye matokeo mazuri katika makundi hayo mawili (best loser) kwa hiyo zinakuwa timu tisa.
Hizo timu tisa za juu zitacheza ligi nyingine kutafuta bingwa atakayeshiriki kuiwakilisha Ujerumani katika makombe mbalimbali ya kimataifa halafu timu tisa nyingine za chini zinacheza kwa ajili ya kupigania kutoshuka daraja ambapo timu mbili za chini zitashuka daraja na tatu tatu ya juu itacheza play-off.
Baada ya timu tisa za kucheza kupata timu nne za juu imeshauriwa kwamba hizo timu nne za juu kwa sababu ligi itakuwa imeisha mapema na haitokuwa jambo zuri wachezaji kukaa hivihivi wakati timu zao zinashiriki mashindano ya kimataifa hivyo itachezwa tena play-off kitu ambacho kiliungwa mkono na makamu wa rais wa zamani wa DFB.
Kwa maana hiyo raundi ya pili ya timu tisa zitakazogombea ubingwa itafanya bingwa wa ligi asitangazwe mapema kwa sababu mbio za ubingwa zinakuwa zinaanza upya.
Kocha wa FC Bayern amesema hiyo haitokuwa sahihi wajaribu kuangalia timu nyingine zitajitahidi vipi kwa sababu mchezo ni kushinda kwa nini timu nyingine zinashindwa kushinda.
Wadau wengi wa soka nchini Ujerumani wametafsiri maoni ya Effenberg kama yanalengo au dhamira ya kuuangusha ufalme wa FC Bayern.

No comments