UDART YASITISHA KWA MUDA HUDUMA YA USAFIRI MABASI YA MWENDO KAS
Kampuni ya inayotoa huduma kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka UDART, inaujulisha umma kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda kuanzia saa 7:30 mchana wa Alhamis Oktoba, 26, 2017, kutokana na kufungwa kwa Barabara ya Morogoro kwa sababu ya daraja la mto Msimbazi kujaa maji.
Huduma itarejea mara baada ya hali kutengemaa. Tunawaomba radhi abiria wetu kwa usumbufu uliojitokeza.
Hata hivyo, huduma ya mabasi yaendayo haraka iliendelea kutolewa kwa njia ya kutokea kituo cha Gerezani, Kariakoo kwenda Muhimbili.
Deus Bugaywa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, UDART

Post a Comment