HALI YA TAHARUKI YATANDA KWA WANANCHI BAADA YA KUKUTA MZOGA WA KUKU UMEVISHWA SANDA HUKU UKIWA NA MADAWA YA KIASILI
Mzoga wa kuku ambaye amefungwa na sanda kwa maelezo ya wananchi ambao walikuwa Nje ya Nyumba ya Bw Emmanuel Kabodi ambapo ndipo tukio hilo limetokea linalo husishwa na imani za kishirikina. |
Mama Mwenye Nyumba ambapo tukio hilo limetokea Bi,Scolastica Nicodemo akizungumza na moja kati ya viongozi wa dini wakati alipofika kwenye familia hiyo kuona tukio hilo la kusitajabisha. |
Baadhi ya wananchi wakishangaa jambo ambalo limetokea katika mtaa wa 14 kambarage. |
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye Nyumba hiyo. |
Baadhi ya watu wakishangaa tukio hilo la kusitajabisha. |
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita wamejikuta wakipigwa na Butwaa baada ya kukuta mzoga wa kuku ukiwa umevishwa sanda kwenye familia ya Emmanuel Kabodi.
Mama wa familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa wakati akifanya usafi aliona nyuma ya geti kuna kitu kimefungwa na shuka jeupe na alipojaribu kukiangalia aligundua ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.
Askofu wa kanisa la TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda ameihasa jamii kuachana na maswala yanasosadikiwa kuwa ni ya kishirikina kwani vitendo hivyo havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .
Mjumbe wa Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata,amesema tukio hilo ni mara ya pili kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la kufukuliwa kwa mtoto na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya vitendo hivyo kuachana navyo mara moja kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo hawataweza kumvumilia.
Wananchi ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho kutokana na matukio hayo kuendelea kujitokeza mara kwa mara.
Mtaa wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na vitendo vinavyosadikiwa ni vya Imani za kishirikiana vya mara kwa mara na kusababisha hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.
PICHA NA MAELEZO NI KUTOKA MADUKA ONLINE
PICHA NA MAELEZO NI KUTOKA MADUKA ONLINE
Post a Comment