Header Ads

Godbless Lema Nae Kamjibu IGP Sirro

Mbunge  Godbless Lema amefunguka na kusema maneno aliyosema IGP Sirro jana kuhusu dereva wa Lissu ni dhihaka kubwa kwa ndugu wa Lissu, wanachama wa CHADEMA na hata viongozi wa chama hicho na kusema hakustahili kusema maneno yale kama IGP.

Lema amesema hayo baada ya IGP Sirro kusikika katika baadhi ya vyombo vya habari akiwa Mtwara akisema kuwa dereva wa Tundu Lissu ndiyo anachelesha uchunguzi wa sakati hilo hivyo aliomba arudi ili kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa ili kufanikisha upelelezi wa sakata la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

"Kamanda Sirro amesikika akiwa Mtwara akisema jeshi la polisi linamuhitaji dereva wa Tundu Lissu kwa ajili ya kukamilisha mahojiano ya upelelezi na kwamba tunasema au CHADEMA inasema anaumwa wakati dereva akionekana akipiga picha anang'ara kabisa, hii ni lugha ya mzaa na lugha ya kadhia hasa kwa familia na sisi wanachama wenzake na Tundu Lissu na hasa kwa dereva mwenyewe ambaye alishuhudia na kusikia milio ya risasi zaidi ya 30 na leo si tu kwamba anatatizo la kisaikolojia kwake binafsi lakini amuona boss wake, kaka yake na mzee wake wa siku nyingi akiwa kitandani akisubiri kudra za Mwenyezi Mungu kuweza kuishi hivyo hii ni kauli ya mdhaa ni kauli ambayo haikupaswa kutolewa na IGP" alisema Lema

Mbali na hilo Lema amelitaka jeshi la polisi kukamilisha kwanza upelelezi wa matukio ya kupotea kwa Msaidizi wa Mbowe, Ben Sanane kifo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ambao wao hawakuwa hata na madereva lakini mpaka sasa jeshi la polisi limeshindwa kutoa ripoti juu ya matukio hayo.

"Leo wanaposema dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi kukamilika siyo kweli kwa sababu Ben Sanane hakuwa na dereva na mpaka leo hatujawahi kuona mchakato wa suala lake kukamilika, Mawazo pia hakuwa na dereva lakini mpaka leo tunaushuhuda kwamba waliopo jela walishawahi kugoma barabarani na kusema wao hawakuwa wahusika wa tukio lile, wapo watu wengi wa CHADEMA wameuwawa lakini hawakuwa na madereva kama wameshindwa kukamilisha kwanza upelelezi huo ni mtake kwanza Sirro akamilishe kwa haraka suala la Ben Sanane ambalo kimsingi wamekataa kufanya utafiti wake, tunajua serikali haiwezi kufanya uchunguzi wa tukio la Lissu kwa sababu wanajua nini kimefanyika" alisema Lema

No comments