AFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MAMBA GEITA.
Kichaka ambacho kipo ndani ya ziwa Viktoria na baadhi ya mitumbwi ya wavuvi ambacho ndicho kinasadikika mamba huyo upenda kujificha kwenye maeneo hayo. |
Ramadhan Dadila ni moja kati ya watu ambao walikuwa na marehemu hapa anazungumza na waandishi wa habari namna ambavyo waliachana wakati wakiwa kwenye shughuli za uvuvi. |
Afisa mtendaji wa Kijiji hicho Bw,Beatus Mazezele akielezea namna ambavyo walipatiwa taarifa ya mtu huyo kushambuliwa na mamba . |
Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kando kando ya vikwe wakisubilia kuanza kumuwinda Mamba . |
Mkazi wa Kata na kijiji cha Bukondo Wilayani Geita Bw Yusufu Samson amemezwa na mamba wakati akiwa katika shughuli zake za uvuvi Oktoba 2.
BAHEBE STAR imefika Kijijini Hapo na kuzungumza na Baadhi ya watu ambao alikuwa nao katika shughuli hiyo ya uvuvi ambapo wameelezea hali ilivyokuwa na hadi umauti ulipomkuta, John Katamla na Ramadhan Dadila,wameelezea kuwa walikuwa naye wakati wa shughuli za kuloa samaki lakini hata hivyo hali haikuwa nzuri hivyo ilibidi wakunje ndoano kwa ajili ya kurudi Nyumbani ingawa marehemu alikuwa anaendelea kuvuta kamba za nanga.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho MAKOYE SOJINGWANONI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema asubuhi wamemwona mamba huyo akitembea maeneo hayo lakini hawakuweza kumfanya lolote hivyo wameomba msaada kutoka kwa mali asili.
Mtendaji wa Kijiji cha Nyansalala,Bw Beatus Mazezele amesema tukio la kukamatwa na mamba mtu sio la mara ya kwanza kwani yamekuwa ya kijirudia mara kwa mara hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuachana na dhana ya kuendelea kuogelea maeneo ya ziwani.
Afisa wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Msese Msese amesema hadi kufikia siku ya jana walipata baadhi ya vipade vya mwili na bado wanaendelea na jitihada ya kuutafuta mwili huo pamoja na mamba ambaye amekuwa ni tishio kwa wananchi wa maeneo hayo.
Post a Comment