Header Ads

Waziri Kindamba Ateuliwa Kuwa Afisa Mtendaji Mkuu Wa TTCL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi wa Bw. Waziri Waziri Kindamba umeanza tarehe 04 Julai, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Waziri Waziri Kindamba alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

06 Julai, 2017

No comments