Header Ads

Rais Magufuli Afungua Barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga imegharimu Sh 190 bilioni.

Waziri Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu ambao wamehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya  kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.

Akizindua ujenzi wa barabara hiyo leo Rais John Magufuli amesema kwamba Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umasikini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.

Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.



No comments