WATU 2 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA VIOO VYA MADIRISHA WALIPOKUWA WAKIVISHUSHA KWENYE GARI MWANZA.
Watu
wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya kuangukiwa na vioo vya madirisha na
milango wakati wakifanya kazi ya kuvishusha kutoka kwenye gari kubwa la mizigo
aina ya semi tela katika eneo la mkolani jijini Mwanza.
Tukio
la kufariki dunia kwa vibarua hao waliofahamika kama Joachim Shija mkazi wa
Igogo na mwenzake aliyetambulika kwa jina la Leonard Maige mkazi wa mabatini
jijini Mwanza, limetokea hii leo majira ya saa nane mchana katika eneo la
Mkolani Centre.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishna wa polisi Ahmed Msangi akizungumza kwa
njia ya simu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, kazi ya kushusha vioo hivyo kutoka kwenye lori lenye namba
za usajili T 844 CSK na tela lake lenye namba T 197 CFE linalomikiliwa na Said
M. Said wa Manyoni mkoani Singida ilianza majira ya saa tano asubuhi, kazi hiyo
ilikuwa inafanywa na vibarua kumi.
ITV
imeshuhudia vioo vilivyokuwa vikishushwa kwa ajili ya kuingizwa kwenye stoo
vikiwa vimevunjika vipande vipande baada ya semi tela hiyo kutikiswa na kuhama
kwenye jiwe lililokuwa limeshikilia stendi yake.
SOURCE:ITV

Post a Comment