Serikali yatoa siku 30 kwa wachimbaji wadogo Mwasabuka kuondoka.
Zaidi
ya wachimbaji wadogo 300 waliovamia eneo la mwekezaji katika eneo la Mwasabuka
wilayani Nyanhwale Geita wameamriwa kuondoka katika eneo hilo ndani ya siku 30
na kujiandikisha katika vikundi ili taratibu za kupewa maeneo mengine ya
zifanyike.
Maagizo
hayo yametolewa na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais,Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina wakati alipotembelea
machimbo hayo yaliyopo katika kijiji cha Mwasabuka, kata ya Mwingiro wilayani
ya Nyanghwale Geita.
Naibu
Waziri huyo amejionea uharibifu wa mazingira unaofanywa na mrundikano wa watu
waliovamia eneo hilo lenye leseni ya kampuni uchimbaji wa madini ya Acacia ambao
wanaendesha shughuli za uchimbaji madini kinyume cha sheria na kutiririsha maji
yanayodhaniwa kuwa na madini ya zebaki katika mashamba na visima vya maji
yanayotimika kwa matumizi ya binadamu.
Akitoa
taarifa ya wilaya kwa Naibu waziri huyo, mkuu wa wilaya ya Nyanghwale Bw.Hamim
Gwiyama amesema uvamizi huo unakwamisha maendeleo ya jamii huku mratibu wa baraza
la taifa la usimamizi na uhifadhi wa mazingira (NEMC )Kanda ya ziwa Jamal
baruti akidai kuwa sheria za mazingira haziruhusu ukataji wa miti hovyo wala
uhalibifu wa aina yoyote na mtu mwenye leseni halali hupatiwa leseni kwa
masharti yakutunza mazingira.
Nao
baadhi ya wachimbaji wadogo katika eneo hilo wamemuomba Naibu Waziri waachiwe
eneo hilo wachimbe ili kujipatia ridhiki kwakuwa wao wanachimba juu na
mwekezaji anachimba chini kwa chini na hakuna mwingiliano wowote.
Post a Comment