Header Ads

NYAMA YA NGURUWE YENYE MINYOO YA TEGU YASABABISHA UGONJWA WA KIFAFA,UPOFU MBINGA.


Wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma inakabiliwa na ugonjwa unaotokana na ulaji wa nyama ya nguruwe wenye minyoo ya keni au tegu ambayo haijakaguliwa ambao unasababisha ugonjwa wa kifafa,upofu wa macho na kupooza ambapo kwa vijijini kutokana na kutokuwa na elimu huyahusisha magonjwa hayo na ushrikina.

Wilaya ya Mbinga ni maarufu kwa ulaji wa nyama ya nguruwe maarufu kwa jina la kitimoto ambapo kaimu afisa mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bw. Sostenes Nakamo amesema tatizo hilo ni kubwa zaidi vijijini ambako hakuna maofisa mifugo wa kutosha wa kupima nyama kabla ya kumfikia mlaji.

Tayari baadhi ya wananchi wa wilaya ya mbinga wameripotiwa kuugua ugonjwa unaotokana na ulaji wa nyama ya nguruwe wenye minyoo ya keni.

Kutokana na tatizo hilo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bw.Gombo Semandito amesema halmashauri hiyo imejipanga kutoa elimu ikiwemo usafi na kufanya ukaguzi kwenye machinjio ya nguruwe.

No comments