Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Nyamhanga Suguta Gesaba 78 mkazi wa kitongoji cha Kibeyo Kijiji cha Getenga kata ya Mbogi Wilayani Tarime Mkoani Mara ameamua kujiunga na kuanza darasa la kwanza kwa lengo la kujua kusoma , Kuandika na Kuhesabu ili kuendeleza biashara zake ndogo ndogo za kuuza Ndizi.
Mzee Huyo amesema kuwa hakubahatika kwenda shule kipindi cha ujana wake hivyo alianza mwaka jana kwenda shule ya na akabahatika kufaulu na hivyo ameamua kujiunga darasa la kwanza ili kutimiza ndoto yake kwani Elimu haina mwisho.
|
Post a Comment