JITIHADA ZA UOKOAJI ZAENDELEA HUKO BUHEMBA MKOANI MARA.
Ikiwa Siku ya tatu tangu kuporomoka kwa kifusi katika moja ya shimo linalotumika kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Magunga lililopo Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara zoezi la kuopoa miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mpaka jana imefikia watu wawili.
Tayari watu kumi na watatu wameokolewa ambapo 6 wameruhusiwa kutoka hospitali, wawili wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Musoma na saba katika hospitali ya wilaya ya Butiama.
Awali akitoa taarifa za kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari mkuu wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani butiama BI. ANNA ROSE NYAMUBI amesema hivi sasa shughuli za kuopoa miili ya waliokufa katika ajali hiyo inaendelea.
Mpaka sasa jitihada za uokoaji zimesitishwa kwa muda na kinachosubiriwa ni uingizwaji wa pamp ili kuvuta maji yaliyoweka kizuizi katika sehemu ya kuingilia ndani ya shimo hilo.

Post a Comment