WEZI WA MIFUGO WAIBA NA KUACHA NAMBA ZA SIMU KASAMWA.
Ng'ombe wakinywa maji katika bwawa la Kasamwa,bwawa ambalo binadamu na mifugo hulitumia kwa pamoja.
Wananchi
wa kata ya Kasamwa wilaya na mkoa wa Geita
wameiomba serikali kuchukua hatua za kisheria kuhusiana na swala la wizi wa
mifugo linaloendelea kwa kasi mkoani hapa.
Hayo wameyasema mbele ya mbunge wa viti maalum Geita upendo peneza kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati walipokuwa kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa ng’ombe,mkutano huo ulikuwa na lengo la kusikiliza
kero za wananchi.
Mbunge wa viti maalumu mkoani Geita(CHADEMA) Mh.Upendo Peneza akiwa na aliyekuwa diwani wa Kasamwa Fabian Mahenge.
Akitoa
taarifa hiyo mbele ya mh.Upendo Peneza,
mwenyekiti wa mtaa wa NMC Kasamwa
kwa niaba ya wananchi Bwana Boazi
Mathayo amesema kuwa suala la wizi wa mifugo limekua ni kero kubwa
kwani baadhi ya wezi wa mifugo hiyo wamekuwa wakiacha namba za simu pindi
wanapoiba ili watumiwe fedha ndipo mifugo hiyo iweze kupatikana.
Mathayo ameongeza kuwa wananchi wa mtaa huo wanakabiliwa na
changamoto ya maji hivyo wameiomba serikali
kusaidia kutatua kero hiyo
ilikuwezesha wananchi wa kata hiyo kupata maji salama
Aidha
mheshimiwa Peneza amelaani vikali
vitendo hivyo vya kikatili vinavyozidi kukithiri mkoani hapa na kuwaomba wananchi
kushirikiana kwa pamoja na kutoa taarifa
katika vitengo husika ili kukomesha uhalifu huo pamoja na unyanyasaji wa
wananchi unaoendelea mkoni Geita.
Post a Comment