WATU 4 WAUAWA NA 5 KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI ARUMERU.
Watu
wanne wakazi wa kijiji cha Kandaskiriet kata ya Oldonyosambu wilayani Arumeru
wameuawa na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na askari
wa SUMA JKT ambao ni walinzi wa shamba la miti la serikali la Meru USA Plant.
Akithibitisha
kutokea kwa mauaji hayo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Charles
Mkumbo amesema tukio hilo limetokea Januari ishirini na nne wakati askari hao
wakiendelea na operesheni ya kuondoa mifugo iliyoingia ndani ya shamba hilo na
ndipo walipokutana na kundi la wananchi wakiwa na silaha mbalimbali za jadi
ambao waliwashambulia na wao wakalazimika kujibu mashambulizi hayo.
Wakizungumza
hospitalini Mount Meru walipolazwa majeruhi na miili ya marehemu
kuhifadhiwa,baadhi ya majeruhi akiwemo William Kilangwa,Mathayo Masharubu na
Thobias Lazaro.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Oldonyosambu Raymond Leirumbe akaliomba Jeshi la
polisi kuharakisha upelelezi wa tukio hilo mapema ili kuwaridhisha
wananchi ambao kwa sasa wako kwenye taharuki kubwa ombi ambalo Kamanda Mkumbo
anaahidi kulifanyia kazi haraka akiwataka wananchi hao kuwa na subira.
Post a Comment