Wanaojitangaza kutibu UKIMWI waanza kusakwa
Tume ya Taifa ya Kudhuibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS kwa kushirikiana na vyombo vya dola inatarajia kuanza oparesheni maalum ya kuwasaka baadhi ya viongozi wa dini na waganga na tiba za asili wanaodai kuwa na uwezo wa kutibu ugonjwa wa UKIMWI
Akizungumza na waandishi wa habari mwanasheria wa TACAIDS Elizabeth Mselu amesema sheria namba 27 inayohusiana na masuala ya kinga dhidi ya magonjwa ya Ukimwi iliyotungwa mwaka 2008 inamzuia mtu yeyeote kutangaza kuwa anatibu Ukimwi au ana mkinga mtu asipate Ukimwi.
Amesema zoezi hilo linaanza leo (Jumatatu) kwa kushirikiana na vyombo vya dola katika mkoa wa Dar es salaam na kwa wale wa mikoani watawatumia watu wao katika kufanikisha zoezi hilo ili kuzuia tatizo hilo lisiendelee kujitokeza na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa ambao wakizidiwa hurudi tena hospitali wakiwa na hali mbaya zaidi.
Post a Comment