Mkuu wa wilaya akiendelea kutoa maagizo juu ya taarifa iliyosomwa
Serikali ya Kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita imetakiwa kupeleka taarifa yenye vielelezo kwa mkuu wa wilaya kuhusu matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 51 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Isingiro bila kufuata taratibu zilizokuwa zimewekwa
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl.Herman Kapufi kwenye mkutano mkuu wa kijiji hicho baada ya wataalam wa hesabu za ndani katika Halmashauri ya wilaya kutokubaliana na taarifa ya mtendaji wa kijiji hicho Bw. Samuel Shosha.
“Mwenyekiti wa serikali ya kijiji, mtendaji na serikali yote ambao walikuwa wamepitisha mihtasali yote, Mkaguzi wa ndani, kamati ya ulinzi na usalama tukutane ofisini kwangu tarehe mbili mwezi wa pili muda wa saa tatu kamili lakini mwenyekiti wa kijiji unapokuja uje na mihtasali yote,stakbadhi na nyaraka zote sitaki tena kisingizio lakini pia mnatakiwa mje na daftari ambalo linaorodha ya mali zote zinazomilikiwa na serikali”Alisisitiza Kapufi
Katika mkutano huo,Afisa mkaguzi wa ndani Chacha Marwa amesema fedha zote za serikali zinatakiwa kuwa na vielelezo pamoja na nyaraka zinazoainisha matumizi jambo ambalo halikuzingatiwa
Akifunga mkutano huo,mwenyekiti wa kijiji Bw.Lumumba Salvatory amekanusha matumizi mabaya ya fedha hizo,huku akisema kuwa hali hiyo inachochewa na Itikad za kisiasa ili kukwamisha jitihada za serikali ya kijiji hicho.
|
Post a Comment