Meneja wa Mgodi huo,Guixue Liu,akiwa na Mwanasheria wa Mgodi Huo Frances Kiganga wakiangalia namna kazi zinavyoendelea kwenye mgodi.
SAKATA la watu wawili wanaodaiwa kupigwa na raia wa kigeni wa China akiwemo aliyelazwa katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita limechukua sura mpya baada ya kubainika chanzo chao cha kupigwa ni kuiba mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu na maji walipokuwa wakifanya kazi katika mgodi wa wa dhahabu unaomilikiwa na kampuni ya RZ uliopo katika kijiji cha Mawemeru wilaya na mkoani Geita na siyo kutokana na madai kupandishiwa mishahara.
Tukio hilo limetokea Januari 19 wakati wa zamu ya usiku baada ya mfanyakazi Benedict Lumimi Maduhu kudaiwa kukamatwa akiwa na mawe yanayodhania kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo wakati akiwa zamu usiku na baada ya kukamatwa akiwa na rafiki yake wa karibu Elisha Silivester [26] ambaye naye anatuhumiwa kwa kuiba maji alifanikiwa kukimbia hadi kituo cha polisi cha Nyarugusu kutoa taarifa kuwa yeye na mwenzake walikuwa wakipigwa na wachina baada ya kudai waongezewe mshahara.
Akithibitsha tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema wafanyakazi Bedeicto Lumimi Maduhu walikamatwa na polisi kutoka ndani ya mgodi huo baada ya kukuta tayari amekamatwa na kufungwa kamba na wafanyakazi wengine wa mgodi huo tayari kwa kumpeleka kituo cha polisi cha Nyarugusu pamoja na mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu .
Ameongeza kuwa Elisha Silvesta anayedaiwa kuiba maji yeye ndiye aliyekimbia na kutoa taarifa kituo cha polisi baada ya kufanikiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na polisi baada ya kufika eneo la tukio waliwachukuwa watuhumiwa Benedicto pia wafanyakaza baadhi wa mgodi huo hadi kituo cha polisi kwa mahojinao ikiwa ni pamoja na kuwahoji baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo akiwemo Elisha mwenywe.
''Taarifa rasmi za uchuguzi ni kuwa chanzo cha kupigwa kwao ni kutuhumiwa kwa wizi wa mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu na maji kama nilivyoeleza sisi kama polisi pia baada ya kutokea malalamiko hayo kutoka kwa watuhumiwa pia wanaotuhumiwa tulichukua jukumu la kuwakamata na kuwahoji na kinachoendelea sasa ni mchakato wa kukusanya ushahidi kwa hatua za kisheria hivyo chanzo ni cha wao kupigwa ni kutuhumiwa na siyo madai ya nyongeza za mshahara”alidai Mponjoli.
Hata hivyo polisi imebainisha wazi kuwa zipo changamoto kwa baadhi ya watu kujenga hoja zinazolenga kujipatia
fedha kutoka kwa wachina kwa kujenga hoja ya kupigwa na kujeruhiwa vitendo alivyodai polisi haina budi kuyafanyia kazi kwa umakini madai hayo kwa vile tayari ipo mifano ya matukio ambayo yaliwasilishwa lakini yakaisha kwa walalamikaji kudai pesa na kutelekeza kesi zao.
Ametoa mfano tukio lililotokea julai 6 mwaka jana la Masanja Shilomero[25] mkazi wa kijiji Nyamitondo kudai kushambuliwa na wajiri wake ambao ni raia wa china na kufunguliwa kesi namba CC/278/2016 mlalamikaji aliitelekeza kesi hiyo baada ya kudaiwa alikuwa ameomba na kupewa fedha kutoka kwa walalamikiwa na kuitelekeza kesi yake.
Kesi hiyo kushindwa kuendelea na siyo kwamba imetelekezwa na polisi,na tukio jingine amelitaja kuwa ni mchimbaji Richard Kasubi anayelalamikiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya kwake kazi ya kushusha mifuko ya saruji kutoka katika gari kuiweka katika
ghala lake badaye walidai kudhurika hata hivyo tayari inadaiwa walilipwa pesa na mlalamikiwa huyo baada ya kutaka malipo kwa ajili ya matibabu na baada ya kiasi cha shilingi 500,000 wanachodaiwa kupewa kukimaliza walianza tena kudai upya na hivyo kuibua mgogoro.
kutokana na uwepo wa mazingira ya aina hiyo polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zote na kuwa Benedicto na wenzake tayari amefunguliwa kesi ya wizi wa mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu katika kituo cha polisi cha Nyarugusu na upelelezi wake unaendelea ikiwemo wanaodaiwa kuwapiga nao wamefunguliwa kesi na inachunguzwa.
Awali akizungumzia matukio hayo Meneja wa mgodi huo wa RZ Gui Xue Liu kupitia msemaji wa kampuni hiyo Francis Beatus Kiganga amesema vitendo vya wizi kwa wafanyakazi wanavyofanya na kisha kuwageuzia kibao kunaweza kuwakatisha tama kuwekekeza katika sekta hiyo ya madini kwani imekuwa ikiwapa usumbufu mkubwa.
Amesema kwa kawaida wao wamekuwa wanapowakamata watuhumiwa huamua kuwafukuza kazi badala ya kuwapeleka
kwenye vyombo vya sheria ili kuepuka kupoteza muda na usumbufu na watuhumiwa kutumia mwanya huo huwageuzia kibao hatua waliyodai inaonekana kuwaathiri na kuiomba serikali kulifanyia kazi kwa umakini wimbi hilo la wachina kutuhumwia kupiga watumishi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Elias Hambuhambu amethibitisha juzi jioni kwa Elisha Sivesta kulazwa hospitalini hapo kwa madai ya kupigwa na kuwa hata hivyo hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na alikanusha uwepo uvumi wa kujeruhiwa sehemu za siri za majeruhi huyo kwani alikuwa amewekewa mpira wa haja ndogo kama hatua ya kawaida kwa wagonjwa wanaolazwa wanaokuwa na madai ya kusikia maumivu ya mwili.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo wakiwemo Amani Silivesta na Annicent Masanja walidai mwenzao elisha aliondoka kwenda kuropiti Kituo cha polisi akijihami baada ya Benedicto kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu wakati alipokuwa zamu ya usiku na waliondoka na Polisi baada ya yeye kwenda kutoa taarifa na wakati huo wote hakuwa amepigwa na madai ya kupigwa yamejitokeza siku mbili baada ya kutokea uhalifu huo hivyo kuibua sintofahamu.
Akizungumzia tuhuma hizo Elisha Silvesta akiwa wodini alimolazwa juzi katika hopitali teule ya mkoa wa Geita alikiri kuwa chanzo cha wao yeye na Benedicto kupigwa ni kutuhumiwa yeye kuiba maji na mwenzake Benedicto kuiba mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu na baada ya kufanikiwa kukimbia alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi Nyarugusu kuwa mwenzake Benecto Lumimi Maduhu alikuwa amefungwa kamba akipigwa bakora na wachina ili kujihami.
|
Post a Comment