RC MARA AKATAA CHAKULA CHA MSAADA
Serikali
mkoani Mara imetangaza kutohitaji hata chembe ya chakula cha msaada baada ya
kujiridhisha kuwa mkoa huo una chakula cha kutosha na kwamba baadhi ya
wanasiasa waache kuhusisha upungufu wa aina ya chakula katika baadhi ya familia
kuwa ni baa la njaa.
Kauli
hiyo imetangazwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa,wakati akielezea
hali ya chakula mkoani humo,na kusema kuwa kuna tabia ya baadhi ya watu wa mkoa
wa Mara wamekuwa wakibagua aina ya vyakula na hivyo kutafasiliwa kuwa mkoa huo
kuwa sehemu ya maeneo yenye uhaba wa chakula nchini.
Kwa
sababu hiyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,amesema katika kuhakikisha mkoa huo
unajitoleza kwa chakula wakati wote, hivi sasa serikali ya mkoa inakamilisha
mipango mbalimbali ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya Ziwa
victoria,mito na mabonde.
Nao
baadhi ya wauzaji wa nafaka katika masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
mkoani Mara,wakitoa taarifa kwa mkuu huyo wa mkoa wa Mara,wamesema kuwa chakula
kipo cha kutosha katika masoko ingawa mzunguko mdogo wa fedha umesababisha
ugumu wa maisha.
Post a Comment