RAIS DKT.MAGUFULI AONDOKA NCHINI KWENDA ETHIOPIA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 28
Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako
atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja
wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais
Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa Bw. Paul Makonda.
Pamoja
na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana
na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria
Mkutano huo.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Mhe. Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki tangu aingie
madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 05 Novemba, 2015
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
28
Januari, 2017
Post a Comment