Header Ads

Picha: Mrirthi wa Kanumba Aunguzwa na Kemikali Usoni

Kumekuwa na tatizo kubwa katika mfumo mzima wa uandaaji wa filamu hapa Tanzania hasa katika suala la kuandaa wasanii ili kuleta uhalisia wa kazi husika.
Kiajana aliyetambulishwa na mama wa aliyekuwa nguli wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kuwa ndiye mrithi wa mwanane huyo kwenye tasnia ya uigizaji, Fred Swai amekumbwa na balaa ambalo ameeleza kuwa hatolisahau katika maisha yake baada kuunguzwa vibaya na kemikali usoni katika harakati za kuandaa filamu.

Akizungumza kwenye Kipindi maalum cha Exclusive Interview kupitia Global TV Online, Swai amesema kuwa siku hiyo aliitwa kwenda kucheza kipande cha muvi ambacho alitakiwa aigize kama mgonjwa.
Hivyo muandaaji alimtaja afungwe bandeji usoni ili kuonesha uhalisia wa mgonjwa, ambapo bandeji hiyo ililowanishwa na kemikali zinazotumika kusafishia vidonda, iodine solution.

Swai aliendelea kueleza kuwa, badala ya kulowanishiwa iodine ya kawaida isiyo kali (diluted solution) aliwekewa concentrated iodine ambayo ni kali zaidi hivyo kuunguza sehemu ya paji la uso.

Hii imekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Muigizaji wa Nigeria, Kuchomwa Moto wakati wakishuti video.

No comments