Header Ads

MITO MITANO MIKUBWA NA HATARI DUNIANI

Mto huu  unapatikana Amerika ya Kusini, ni mkubwa kuliko mito yote duniani na hatari sanaa kwasababu ya urefu wake na upana wake.
Kwakuwa mto huo ni mkubwa kuliko mito yote duniani ulipewa jina jingine ambalo ni "River Sea" likiwa na maana ya  "Mto bahari". Mto huu una kina zaidi ya futi 50 na ni mkubwa kiasi cha kutokuwa na uwezo wa kupatikana sehemu za kuungia daraja kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
2. MTO CONGO
Mto huu uliofahamika kwa jina la Zaire miaka ya nyuma unapatikana Afrika ya Kati nchini Congo, una urefu wa maili 2992.
Mto huu ni hatari sana kwasababu ya kasi ya maji yake ambayo huanza taratibu na kuongeza kadri maji yanavyozidi kutiririka.
Ukizidi kutiririka huchukua kasi kubwa sana kiasi cha kuufanya mto huo kuwa na nguvu sana kabla haujaingia Geti la Kuzimu "Gates of Hell" amabalo ni korongo lenye urefu wa maili 75, lenye kumwaga maji kwa haraka sana. Kwasababu hii mto huo umekuwa na sifa ya kuwa mto wa kwanza wenye nguvu Afrika.
3. MTO ORINOCO
Mto huu unapatikana Amerika ya kusini ukiwa na sifa ya kuwa mto wa tatu kwa urefu wa maili 1330 barani humo.
Mto huu unaotiririka kupitia Colombia na Venezuela una hatari kubwa kwasababu kusini magharibi ya mto huo kumefunikwa na pori kubwa ambalo huufanya sehemu kubwa ya mto huo kutokuonekana.
4. MTO YANGTZE

Huu ni mto unaopatikana China, ulio na sifa ya kuwa mto mrefu barani Asia na nchi ya China. Mto huo una urefu wa maili 3964 na unamwaga maji yake katika bahari ya Mashariki ya China  (East China).
Mto huo una hatari sana sababu ya kuwa na kasi kubwa ya maji na gogi katika mtiririko wake. Mawimbi ya mto huo yana nguvu sana sababu inayopelekea mara nyingi kutokea mafuriko katika mto huo.
5. MTO BRAHMAPUTRA


Mto huu wenye chanzo chake Tibet ya kusini magharibi, una urefu wa takribani maili 1800 ukitiririka kupitia Tibet, China, India na Bangladesh.
Hatari ya mto huu ni mafuriko makubwa ambayo hutokea pale barafu ya milima Himalaya inapoyeyuka na pia kwasababu ya nguvu ya mawimbi yake.

No comments