KICHANGA CHATUPWA CHOONI GEITA.
Matukio ya watoto kutupwa yanaendelea kuchukua sura mpya baaada ya tukio jingine kutokea leo katika mtaa wa Msalala road Geita mjini ambapo mtu asiyejulikana ametupa kichanga katika shimo la choo jirani na Mbeho Guest house.
Kichanga hicho kimegundulika kuwa kimetupwa chooni baada ya dada mmoja(jina linahifadhiwa) jirani na eneo hilo kukuta hali ya shimo hilo ni tofauti na ilivyokuwa kawaida kwani siku zote limefunikwa lakini alishangaa kukuta lipo wazi wakati akianika nguo ndipo aliposogea na kuchungulia akaona mfuko mweupe ndani ya shimo,alichukua mti na kukagua vizuri ndipo alipogundua kuwa kuna mtoto na kuamua kuwaita majirani pamoja na mama mwenye nyumba(jina tunalihifadhi).
Tayari polisi wamefika eneo la tukio na kukichukua kichanga hicho na upelelezi wa nani kafanya tukio hilo unaendelea.
Post a Comment