KAPUFI:MSISUBIRI SERIKALI IFANYE KILA KITU.
Mkuu
wa wilaya ya Geita Mwl Herman Immakulata Kapufi amewataka wananchi wa kata ya Rwamgasa
kuendelea kujitolea katika suala la kuchangia maendeleo na kuacha tabia ya kuitegemea serikali kwa kila kitu.
Ameyasema
hayo wakati alipokuwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Rwamgasa Wilayani hapa uliokuwa na
lengo la kusikiliza kero za wananchi.
Mkuu
huyo wa Wilaya ameiomba jamii kushirikiana na serikali hasa katika miradi ya
maendeleo pamoja na elimu.
“Na
hasa hapa Rwamgasa kuna changamoto nyingi,changamoto ya kwanza ni changamoto ya
elimu,nilikuwa nipo pale shule ya msingi Mwenge ina madarasa nane ina nyumba za
walimu mbili ina walimu 22 inahitaji madarasa 36 lakini ina madarasa 8 na ina
upungufu wa madawati 222.”Alisema DC Kapufi.
Hivi
karibuni kulikuwa na zoezi la uchangiaji wa madawati ambalo baadhi ya watu
walijitoa kwa moyo wa kupenda lakini bado changamoto ni kubwa hasa katika vyumba
vya madarasa ikizingatiwa kuwa mwaka huu ni idadi kubwa ya watoto
walioandikishwa kujiunga na darasa la kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma,na
hii ni kutokana na sera ya serikali ya awamu ya tano ya Elimu bure.
Post a Comment