Donald Trump kawafuta kazi Mabalozi wote wa Marekani duniani.
Kwa mujibu wa The Independent na ParsToday wanasema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.
Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo kawaida.
Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.
Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya kuanza kazi zao.
Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na haya yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa kiongozi huyo.
Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa Marekani.
Post a Comment