BINTI AJIFUNGUA NA KUTUPA MTOTO KATIKA CHOO CHA KANISA SHINYANGA.
Binti
mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 23 anashikiliwa na Jeshi la polisi
mkoani Shinyanga kwa kosa la kujifungua mtoto na kumtupa katika shimo la choo
cha kanisa eneo la Kitangili mjini Shinyanga hali ambayo imesababisha kifo
chake.
ITV
imefika katika eneo la Kitangili mjini Shinyanga na kukuta kundi kubwa la watu
wakiwa katika hali ya taharuki wakilalamikia kitendo kilichofanywa na binti
huyo huku wakieleza masikitiko yao kwa kitendo cha kutupwa mtoto ambapo
mchungaji wa kanisa la AIC Kitangili ambako tukio limetokea akieleza kuwa yeye
na baadhi ya waumini waligundua kuwepo kwa mtoto mchanga katika shimo la choo
baada ya kusikia akilia.
Kaimu
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Elias Mwita amekiri kutokea kwa tukio
ambapo amesema chunguzi wa awali unaonyesha kuwa binti huyo anahusika lakini
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.
SOURCE:ITV.
Post a Comment