Header Ads

AUAWA BAADA YA KUKAMATWA AKIVUNJA AMRI YA SITA.

Image result for KUFANYA MAPENZI

Mwanaume mmoja mkazi wa  Igunga mkoani Tabora  ameuawa na kundi la wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. 

Akizungumza juzi mjini Tabora, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani amesema katika tukio la Januari 28, mwaka huu katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga Mjini, mkazi wa Mtaa wa Masanga, Khalid Kassim (50) aliuawa na kundi la wananchi zaidi ya 100 ikidaiwa alifumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu.

Kamanda Selemani amefafanua kuwa Kassim alifumaniwa na mwenye mke, Muungano Isaack (44) mkazi wa Mtaa wa Stoo.

Amesema baada ya kumfumania, Isaack alipiga kelele kuomba msaada, ndipo wananchi walitoka kwa wingi na kumshambulia kwa kipigo Kassim.

Amebainisha kuwa polisi walipata taarifa na kufika katika mtaa huo na kukuta wananchi wakiwa wamekimbia, hivyo askari walimchukua mtuhumiwa na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu.


No comments