Al-Shabaab wauwa 7, wajeruhi 20 Mogadishu.
Watu saba wameuwawa na 20 kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabaab kuivamia hoteli moja mjini Mogadishu kwa magari yaliyojaa mabomu.
Polisi na watu walioshuhudia wamesema leo kwamba mripuko wa kwanza ulitokea katika lori lililokuwa limewekwa miripuko karibu kabisa na sehemu ya mbele ya hoteli hiyo, wakati mripuko wa pili ulikuwa wa bomu lililowekwa ndani ya gari iliyokuwa imeegeshwa karibu na hoteli.
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabaab walivamia hoteli hiyo ya Dayah, ambayo inatembelewa zaidi na wafanyabiashara na maafisa wa serikali baada ya shambulio hilo la mabomu.
Afisa wa Usalama, Mohammed Hassan, amesema idadi ya watu waliouwawa inatarajiwa kupanda kwa sababu baadhi ya watu huenda wamenaswa ndani ya hoteli hiyo yenye ghorofa tatu.
Watu wengine 20 wamejeruhiwa kwa mujibu wa polisi.
Post a Comment