Header Ads

Trump aitaka Marekani kuboresha silaha za nyuklia


Donald Trump ameitaka Marekani kuboresha zaidi uwezo wake wa zana za nyuklia.

Rais huyo mteule ambaye ataingia ofisini mwezi ujao amesema kuwa Marekani ni lazima ichukue hatua kama hizo, hadi wakati ulimwengu utatathmini suala la nyuklia.

Trump aliyazungumza hayo saa kaadha baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa Urusi inahitaji kuboresha uwezo wake silaha za nyuklia

Marekania ina silaha 7,100 za nyuklia huku Urusi ikiwa inamiliki silaha 7,300 kulingana na shirika la kudhibithi silaha la marekani.

Trump aliyaandika hayo kwenye akaunti yake ya mtando wa twitter

Wakati wa kampeni, Trump alisema kuwa silaha la nyuklia ndilo tatizo kubwa zaidi linaloikumba dunia.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton mara kwa mara alimtaja Trump kuwa mtu asiye na uvumilivu wa kuweza kuzuia vita vya kinuklia.

Putin anasema Urusi ni imara kuliko hasimu wake yeyote.

No comments