Header Ads

Ofisa Mtendaji wa Kata Mbaroni kwa Kubaka Mwanafunzi Darasa la Tatu

MWANZA: Jeshi la Polisi Mkowa wa Mwanza wanamshikilia Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, Bwana James Chiragwire kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 12.

Habari zilizopatikana kutoka shule anayosoma mtoto huyo na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Oscar Msuya tukio hilo lilitokea juzi Novemba 17, 2016 baada ya walimu kubaini matatizo ya kiafya ya mwanafunzi huyo aliyeshindwa kuingia darasani na kulala nje ya uzio wa shule.

No comments