Header Ads

MMCHUNGAJI ATUMIA DAWA YA MBU KUFANYA MIUJIZA.


Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.

Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook,mchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua wadudu inayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.

Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.

Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.


Nchi hiyo imekuwa na wimbi la visa ambapo wajumbe wa kanisa wamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.

Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mount zion General Assembly katika jimbo la Limpopo ,anaonekana akimpulizia dawa ya kuua wadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.

Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwa sababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".

Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.

Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi  mchungaji aliyejitangaza kuwa ''nabii'' huko Limpopo - Lethebo Rabalogo kuacha kupuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:

''Tunaona tendo hili  linatia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu''.

''Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwaua wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo , na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.''

''Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo'' imesema kampuni ya Tiger.

No comments