Madeni ya benki, Vicoba Saccos kilio kipya mtaani
Hoteli Tai Five iliyo jijini Mwanza imewekwa mnadani kufidia deni baada ya mmiliki kushindwa kulipa mkopo aliokopa CRDB.
Ndivyo unavyoweza kuelezea hali ya uchumi ya wananchi kwa sasa.
Wengi walitegemea mikopo kutoka benki, Vicoba na Saccos kama mtaji wa kuanzisha biashara au kuimarisha biashara, lakini hali imebadilika tofauti na matarajio yao na sasa marejesho yamekuwa mzigo mkubwa, huku madeni yakidhoofisha taasisi za kifedha.
Wakati hao wakiangusha kilio hicho, wachache wanaweza kuneemeka; kampuni za udalali zinapata zabuni za kufuatilia wadaiwa sugu na vyombo vya habari vinapata fedha kutokana na matangazo ya kuwasaka wakopaji hao waliotoweka na fedha za benki na taasisi nyingine za fedha.
Hali hii imetokea katika kipindi cha mwaka mmoja na kuibua mjadala mkubwa ulioingia hadi bungeni wakati wa kupitisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2017/18 ambako wabunge wa chama tawala na upinzani waliungana kukosoa uendeshaji uchumi, wakidai kuwa ndio umesababisha hali mbaya kwa wananchi.

Post a Comment