WAUMINI WATINGA KANISANI NA MABANGO KUMPINGA ASKOFU.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki wakiwa na mabango walipohudhuria ibada kwenye Kanisa Kuu la Mtwara jana. Picha na Haika Kimaro
Hata hivyo, Askofu Mbedule amesema asingependa kuyazungumzia suala hilo kwa sababu walikaa kikao.
Umoja wa wazee ulitoa tamko ndani ya kanisa hilo kutokana na tuhuma zinazomkabili askofu huyo na kumtaka asijihusishe na mambo yanayohusu usharika na dayosisi, ili kupisha uchunguzi na kumwomba Mkuu wa KKKT, Dk Fredrick Shoo kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo.
Akisoma tamko la wazee wa kanisa hilo, Amon Mkocha amesema wanapinga uamuzi uliofanywa na kikao cha halmashauri kuu kilichofanyika mwezi huu.

Post a Comment