Header Ads

Video: Samatta aanza kutupia kwenye Europa

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta amefanikiwa kufunga goli lake la kwanza kwenye mchezo wa awali wa kuwania kufuzu kucheza Europa.
Samatta
Timu ya Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Buducnost Podgorica ya nchini Montenegro.
Magoli ya Genk yalifanikiwa kufungwa na Neeskens Kebano aliyefunga goli la kwanza dakika ya 17 kwa njia ya penalti na baadaye kwenye dakika ya 79 Samatta alifanikiwa kufunga bao la pili.
Tazama video ya goli la Samatta hapa.


No comments