Header Ads

Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle Obama


Melania
Sherehe ya ufunguzi wa kongamano kuu la wajumbe wa chama cha Republican nchini Marekani imegubikwa na utata baada ya hotuba iliyotolewa na mke wa Donald Trump.

Hotuba hiyo ya Melania inadaiwa kuwa na maandishi yaliyotolewa kutoka kwenye hotuba ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle, aliyoitoa miaka minane iliyopita.

Mke huyo wa Trump, ambaye ni mzaliwa wa Slovenia, amesema alipata usaidizi mdogo sana wakati wa kuandika hotuba hiyo, ambayo imesisitiza sana maadili ya kifamilia na kujumuishwa kwa watu wa matabaka yote.
Maafisa wa kampeni wa Bw Trump hawajajibu madai hayo.
Wengi wa waliohutubu katika kongamano hilo linaloendelea mjini Cleveland, Ohio, wameangazia sana kutilia shaka uwezo wa mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa rais.
Meeya wa zamani wa New York Rudy Giuliani amewauliza wajumbe: “Nani anaweza kumwamini Bi Clinton amlinde?”
Awali, wajumbe wanaompinga Bw Trump waliandamana na kulalamika baada yao kuzuiwa kuwasilisha pingamizi zao.

No comments