Utendaji wa Mkuu wa Wilaya Wakwaza Madiwani Morogoro
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogorowamesa hawajaridhishwa na utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, John Henjewele kushughulikia migogoro ya ardhi inayoendelea wilayani humo.
Waliyasema hayo katika mkutano na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi wilayani humo.
Diwani wa Mbigiri, Juma Rajab alisema amejaribu kufika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kuhoji uhalali wa mashamba kuendelea kushikiliwa na wawekezaji hewa ambao hawayaendelezi, lakini hapati ushirikiano.
Diwani wa Kata ya Makole, Anfas Kaunda alimueleza Lukuvi kuwa kuna shamba namba 35 lililopo Kijiji cha Mambeya ambalo lilifutiwa hati na kurejeshwa serikalini tangu 1984, lakini hadi leo halijakabidhiwa kwa kijiji.
Akizungumza baada ya mkutano, Henjewele alisema diwani huyo ana mgogoro na wananchi wake ambao amewakodisha mashamba ya Serikali kwa gharama kubwa.
Post a Comment