PICHA:Mama Magufuli amshukuru Mtumishi wa Mungu TB JOSHUA kwa kuunga mkono Jitihada zake za kusaidia wazee
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na
Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo
cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi
pamoja na Vifaa vya Malazi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongozana
na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima
Dendegu baada ya kuangalia nyumba zinazojengwa na kufanyiwa marekebisho kwa
ajili ya makazi ya wazee wa kituo cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini
kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka
Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi, Madawa pamoja na
Vifaa vya Malazi.
Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akisaini
kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka
Mkoani Mtwara
Baadhi
ya Wazee walimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Janeth Magufuli
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akimueleza
jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu
wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akicheza
ngoma na moja ya kikundi cha kinamama Mkoani Mtwara wakati wa hafla ya utoaji wa
misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani
Mtwara.
Kaimu
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi
Kambona akiwashukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth
Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary
Majaliwa kwa kutambua umuhimu wa kusaidia wazee katika kituo hicho na kutoa
misaada itakayowapunguzia machungu ya mahitaji maalum wazee hao.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw.
Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akiongea na wazee na baadhi ya watu
waliojitokeza katika hafla ya utoaji Misaada katika kituo cha kulea Wazee cha
Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa
misaada hiyo na kumuahidi kusimamia ugawaji wa vitu hivyo ili kuepuka
kuchukuliwa na watu wasiowaaminifu.
Muwakilishi
wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua Nchini Tanzania akitoa salamu kutoka kwa TB Mhandisi
Consolata Ngimbwa Joshua aliyetoa msaada kwa ajili ya wazee wa kituo cha
Nkaseka kilichopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na
wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru Mtumishi wa Mungu TB
Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa
kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.
Kiongozi
wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Bw. Boniface Mbedo akiwashukuru
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa kwa misaada
waliyotoa na uamuzi wa kukitembelea kituo hicho.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia
jambo na moja ya Mzee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka baada ya kumpa
zawadi ya Ungo, Chungu na Mwiko. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa, wakati wa hafla ya utoaji misaada
kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia
jambo na baadhi ya watoto waliojitokeza katika hafla ya utoaji msaada katika
Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
















Post a Comment