Mfugaji Geita auza ng’ombe 3,000 na kujenga hospitali.
Moja ya story ambayo imeandikwa June 11 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘Mfugaji auza ngombe 3000, ajenga hospitali ya sh bil 2 Geita‘
Mfugaji Makoye Athuman, mkazi wa Mtaa wa Tambukareli, kata ya Kalangalala mkoani Geita ameuza ng’ombe 3000 wenye thamani ya bil 2.1 na kujenga hospitali ya kisasa katika eneo hilo.
Gazeti hilo limeeleza kuwa mfugaji huyo maarufu kwa jina la Makoye Meno, alisema alichukua uamuzi huo baada ya kuguswa na ukosefu wa huduma za afya katika eneo hilo na aliamua kuwekeza kwenye sekta hiyo pamoja na kuondokana na migogoro ya wakulima na wafugaji. Athuman alisema hospitali hiyo itakuwa na wataalamu wa magonjwa mbalimbali na baadhi ya madaktari bingwa kutoka nchini India.
Post a Comment